Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Wednesday, October 17, 2012

DK ULIMBOKA ATOA YA MOYONI; ASEMA ALIYEMPIGIA SIMU NI RAMADHANI IGHONDU

 
 
Dk. Stephen Ulimboka siku alipowasili nchini akitokea Afrika Kusini kwa matibabu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka leo ameeleza ya moyoni baada ya kutoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kupitia kwa wanasheria wake ambao ni Shayo na Nyaroro Kichere. Taarifa hiyo imeeleza kuwa aliyekuwa anawasiliana nae kabla ya kutekwa, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande usiku wa Juni 26 mwaka huu ni Bwana Ramadhani Ighondu ambaye alidaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Katika taarifa hiyo Dk. Ulimboka anaeleza kushangazwa na kutokamatwa mtu huyo mpaka sasa na kudai kuwa yeye yupo tayari kutoa ushirikiano kwa tume huru japo mpaka sasa haijaundwa.


0 comments:

Post a Comment