Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Wednesday, July 4, 2012

MGOMO WA MADAKTARI: STELLA JOEL AFIWA NA KAKA YAKEMWIMBA Injili Bongo, Stella Joel (pichani) ameonja adha ya mgomo wa madaktari nchini kufuatia kufiwa na kaka yake mkubwa, Josia Joel kwa madai ya kukosa matibabu.
Akizungumza kwa majonzi mazito hivi karibuni nyumbani kwake, Ubungo - Msewe, jijini Dar, Stella alisema marehemu kaka yake alikuwa akiumwa na kuzidiwa, akampeleka Hospitali ya Amana, Juni 23 mwaka huu, alipopimwa alibainika kuwa ana tatizo la kifua hivyo daktari aliwataka wauguzi wampeleke wodini ili asubiri matibabu.
“Tulimfikisha marehemu pale Amana Jumamosi, Juni 23, alipimwa na daktari wa zamu na alibaini anasumbuliwa na kifua.
“Lakini cha ajabu alisema apelekwe wodini kusubiri matibabu hadi Jumatatu yake yaani Juni 25.
“Siku hiyo hakupewa dawa yoyote, tukaambiwa turudi nyumbani tumwache mgonjwa. Tuliporudi asubuhi, Juni 24 tulikuta kaka amelala ubavu, tulipomsogelea tuligundua amefariki dunia.
“Tuliwauliza wauguzi kwa nini hawakumuweka vizuri wakasema daktari hakuwepo hivyo wao wasingefanya chochote,” alisema Stella.
Stella alimaliza kwa kusema waliomba ndugu yao akahifadhiwe mochwari, lakini wauguzi wakadai wanasubiri kibali cha daktari hivyo wakaamua kutafuta daktari wanayemfahamu wao na kufanikiwa kuuchukua mwili wa marehemu na kupelekwa kuhifadhiwa mochwari.
“Kwa kweli mgomo huu unaumiza wengi, wahusika wangejaribu kuliangalia upya. Hivi wao hawauguliwi?” alihoji Stella akitokwa machozi.

0 comments:

Post a Comment