Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Tuesday, July 31, 2012

ALIYETAKA KUMUUA MANDELA JELA MAISHA

 Mike du Toit.
Nelson Mandela.

MHUSIKA mkuu wa mpango wa kumuua Nelson Mandela, wiki iliyopita katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo alipatikana na hatia ya uhaini kwenye kesi moja iliyodumu kwa takriban miaka 10 na atahukumiwa jela maisha.
Mike du Toit alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu na kiongozi wa kundi la kibaguzi la Jeshi la Kaburu la Chama cha Boeremeg, baada ya kupatikana na hatia na mahakama kusema atahukumiwa siku zijazo kuhusiana na jaribio lililoshindwa la kumpindua Mandela mwaka 2002 nchini Afrika Kusini, wanasheria akiwemo Steve Mhokholo, wamefunguka na kusema hukumu yake itakuwa kifungo cha maisha jela.
Mashahidi waliieleza mahakama kuwa du Toit na wenzake walipanga kumuua Mandela ambaye mwaka 1994 alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini pia walikusudia kuwapiga risasi weupe wenzao ambao wangepinga mtazamo wao wa kuwa taifa kamili la kibaguzi la Makaburu.
Du Toit alitaka kukiondoa madarakani kwa nia ya mapinduzi chama tawala cha African National Congress (ANC) na mahakama kuu nchini humo imesema atahukumiwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Ilidaiwa kuwa du Toit angefanikiwa kumpindua Mandela angewafukuza Waafrika wapatao milioni 40 kwa kuwalazimisha kwenda kuishi Zimbabwe tena basi wakiwa na vifurushi tu vya chakula na Wahindi wangepakiwa katika boti na kupelekwa kwao India.

0 comments:

Post a Comment