Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Thursday, June 21, 2012

VENGU ATUA BONGO, AFICHWA

   


MUNGU mkubwa lakini madaktari wa Kihindi nao ni noma! Ndivyo alivyoanza kusimulia shuhuda aliyemuona staa wa Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ‘Vengu’ anayedaiwa kutua Bongo kwa siri na kufichwa, Amani limeinyaka.
ALIYEMUONA
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, Vengu aliyekuwa akitibiwa maradhi ya kichwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India tangu mwaka jana, alitua Bongoland hivi karibuni na kufikia nyumbani kwao maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Vengu ambaye alilazwa Hospitali ya Muhimbili tangu Agosti, mwaka jana na baadaye kuhamishiwa India baada ya hali kuwa tete, tangu atimbe nchini amekuwa akifanyishwa mazoezi ya kutembea kwa siri.

“Kuongea anaongea lakini siyo vizuri sana, inaelekea ulimi ni mzito. Mtu ukilazwa karibia mwaka mzima bila kuongea huwezi kunyanyuka tu na kuongea,” alisema shuhuda huyo.
USIRI
Katikati ya Mei, mwaka huu ilidaiwa Vengu angerejea nchini wakati wowote baada ya afya yake kutengemaa lakini ndugu mmoja wa karibu (jina lipo) alisema walipindisha taarifa na kumleta kwa siri kupitia mlango wa VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar.

WENZAKE WANASEMAJE?
Amani lilizungumza na wachekeshaji wenzake juu ya kutua Bongo ambapo baadhi walikiri na wengine kudai hawajui chochote.

SEKI VIPI?
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’ alipopigiwa alisema kuwa hawezi kuthibitisha lolote hivyo Amani liwatafute ndugu wa staa huyo.

AHAMISHIWA KIMARA
Alipotafutwa ndugu wa staa huyo, alidai kuwa kweli Vengu yupo Bongo lakini alihamishwa Mabibo na kupelekwa Kimara, Dar anakoishi na shangazi yake kwa sasa akiendelea na mazoezi ya kutembea.

TURUDI NYUMA
Vengu alikuwa akikabiliwa na ugonjwa uitwao Brain au Cerebral Atrophy. Ugonjwa huu husababisha seli za kichwani kukosa mawasiliano na sehemu nyingine na mgonjwa huzimia mara kwa mara.

0 comments:

Post a Comment