Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Wednesday, June 13, 2012

TANZANIA YAMKAMATA ERDOGAN

 Emrah Erdogan

Mtu mmoja anayeshukiwa kuwa ana uhusiano na shambulio la mwezi uliopita katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi amekamatwa nchini Tanzania. Polisi ya Kenya inasema kuwa Emrah Erdogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki. Kenya inadai kuwa alivuka mpaka mapema mwezi Mayi kutoka Somalia ambako alishiriki mapigano kwa niaba ya kundi la Al Shabab. Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika mlipuko ambao wakuu wa Kenya wanasema ulisababishwa na bomu hilo.


Kumekuwepo na kutofahamika juu ya chanzo cha mlipuko huo ila Maofisa wa Polisi walianza kwa kusema kuwa mlipuko huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme. Mara kwa mara kundi la Al Shabab limetishia kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Kenya kwa sababu nchi hiyo ilituma vikosi nchini Somalia.

Serikali ya Kenya inalituhumu kundi la wapiganaji wa Al Shabab kuhusiana na utekaji nyara wa watu kadhaa kwenye ardhi yake pamoja na kusababisha hali ya wasiwasi kwenye mpaka baina yake na Somalia.

Polisi ya Tanzania imethibitisha kwa BBC kuwa Bw.Erdogan alikamatwa na kuahidi maelezo zaidi baada ya muda mfupi. Erdogan ni miongoni mwa watu wanne ambao Polisi ya Kenya imekuwa ikiwasaka tangu kutokea kwa mlipuko huo.

Bw.Erdogan, anayejulikana pia kama Salahuddin al-Kurdi, inaaminika kuwa aliwahi kusafiri kwenda Waziristan huko Pakistan ya kaskazini magharibi mwaka 2010 ambako alijiunga na kundi la wakereketwa wenye imani kali kabla ya kuelekea Somalia mwaka jana, kwa mujibu wa shirika la habari Reuters.

0 comments:

Post a Comment