Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Thursday, May 31, 2012

Wazee wa EAC kufungua kesi nyingine

Wazee wa EAC
Sakata la wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo ilivunjika mwaka 1977 limeibuliwa upya ambapo sasa wameunganisha makundi yao ili kuiburuza mahakamani serikali wakiidai zaidi ya Sh. bilioni 450.

Ingawa hawakusema ni lini watawasilisha mahakamani madai yao, lakini wakasema juhudi za haraka zinafanyika ili kuhakikisha wanaiburuza serikali mahakamani.

Walisema jana kuwa madai yao yamechukua miaka 35 tangu mwaka 1977 na kwamba muda wote serikali imekuwa ikiwazungusha. Mwenyekiti wa wastaafu hao, Ahmed Kabunga, alisema kabla ya kufungua kesi hiyo wameanzisha mchakato wa kuunganisha vikundi yote.

Alisema mgawanyiko wa wastaafu hao ulichangia kuwadhoofisha walipokuwa wakitoa madai yao kwa serikali na hivyo kujikuta wanashindwa kufanikiwa na kwamba hivi sasa wamebadili utaratibu.

Kwa mujibu wa Kabunga, mwaka 2005 baada ya kukaa na serikali na kufikia mwafaka walitakiwa kulipwa zaidi ya Sh. bilioni 450 na kiasi kingine cha fedhaa ambacho kilikuwa hakikuingizwa katika utaratibu huo.

Alisema mwaka 2003 walifungua kesi mahakamani kabla ya serikali kuwaomba wafanye mazungumzo nje ya Mahakama ambayo yalifanyika na kufikiwa mwafaka kati ya mwaka 2004/2005.

Hata hivyo, Kabunga alisema mwafaka kati yaao na serikali haukuheshimiwa na upande wa pili hatua iliyowafanya afungue kesi nyingine na kwamba tangu wakati huo wamekuwa wakihangaika bila kupata haki yao.

Alisema tangu waanze kudai madai yao wazee wengi wamekata tamaa huku wenzao wakifariki dunia kabla hawajapata haki zao

0 comments:

Post a Comment