Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Thursday, May 24, 2012

Uhamiaji yachunguza madai ya ufisadi


IDARA ya Uhamiaji, inawachunguza watumishi wake wanaodaiwa kuwa na utajiri wa kutisha uliopatikana kwa njia za kifisadi na kwamba ikithibitika hatua za kisheria zitachukuliwa bila kujali vyeo vyao.

Hatua hiyo imekuja baada ya gazeti hili, kuchapisha habari za kuwepo kwa vigogo saba wenye utajiri wa kutisha akiwemo mmoja anayemiliki akaunti za mamilioni ya fedha za kigeni.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Magnus Ulungi, ilisema idara hiyo ilianza kuzifanyika kazi taarifa hizo kabla hata hazijachapishwa gazetini.

“Tunapenda kuufahamisha umma kwamba Idara ya Uhamiaji haina kigogo, watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria,” alisema.

“Idara kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, tunamchunguza mtumishi anadayedaiwa kumiliki akaunti za fedha za kigeni ili kubaina ukweli na kuchukua hatua,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Alisema mtu yeyote atakayethibitika kukiuka sheria, kanuni na taratibu za kazi, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria bila kujali cheo chake.

Kamishna Mkuu alisema kwa upande wa vibali bandia, idara hiyo ilifanya uchunguzi na kuwafikisha baadhi ya watumishi mahakamani.

“ Wapo tuliowafikisha mahakamani na wengine uchunguzi bado unaendelea, idara itafurahi kupata taarifa kama kuna watu wengine wanaoendelea na utoaji wa vibali bandia,” alisema.
Alisema watumishi wa Idara ya Uhamiaji, hawaruhusiwi kupokea fedha za wateja kwani wateja hutakiwa kulipia benki kwa kila aina ya huduma wanayoihitaji.
Akizungumzia uhamiaji haramu, Kamishna alisema vyombo vya ulinzi vimeweka mikakati madhubuti ya kudhibiti uhamiaji haramu.

Maofisa hao saba wanaodaiwa kuchunguzwa kwa ufisadi wanatoka katika vituo vya kazi vya Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.

0 comments:

Post a Comment