Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Thursday, April 26, 2012

USIRI WA KANUMBA ULIFICHA MENGI; ANA WATOTO WENGIPAMOJA na kwamba msanii maarufu, Steven Charles Kanumba amefariki dunia bila ya kujaaliwa mtoto, hali inaonyesha kuwa mambo yanaanza kubadilika kutokana na wanawake kuanza kujitokeza wakidai walizaa naye.
Tayari mwanamke mmoja kutoka Sumbawanga ambaye anaelezwa kuwa aliwahi kufanya kazi ya msaidizi wa ndani kwa Kanumba ameshajitokeza na kutangaza kuzaa na msanii huyo mtoto wa kiume.
Lakini inaelezwa kuna msichana mwingine mkoani Mwanza ambaye ni msomi, tayari ametangaza kuwa na mtoto wa kike aliyezaa na marehemu Kanumba, hali inayoashirikia huenda kuna wengine watajitokeza na kusababishe kuwe na idadi kubwa ya watoto watakaoitwa wa Kanumba.
Huenda kauli ya mama yake Kanumba, Flora Mtegoa kutangaza kuwa anahitaji kuwaona watoto wa mwanaye na kusisitiza wajukuu zake wapelekwe ili awalee inaweza kusababisha wanawake zaidi wajitokeze wakiwa na ‘watoto’ wa Kanumba.
“Nina hofu huenda watoto wakafikia hata kumi, tokea kifo chake haujafika hata mwezi lakini watoto wa Kanumba wanaanza kutangazwa kwa kasi kubwa,” alisema rafiki wa karibu wa Kanumba ambaye ni muigizaji ambaye aliomba kutotajwa.
Pamoja na Mama Kanumba kukaribisha wajukuu zake, ndugu wengine wamegawanyika katika makundi mawili kuhusiana na suala la watoto hao.
Kanumba alifariki usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu na bado chanzo cha kifo chake kina utata kutokana na kuelezwa kilisababishwa na msanii mwingine kina, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye tayari ameshapandishwa kizimbani.

0 comments:

Post a Comment