Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Monday, April 2, 2012

DIAMOND APIGA SHOW KALI, HUKU WEMA SEPETU AKITIA AIBU UKUMBINI


Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpozzz akifanyiwa mahojiano mara baada ya kuwasili kwenye tamasha la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platinum akiwarusha mashabiki waliohudhuria katika tamasha lake la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Diamond akionyesha umahili wake wa kuimba.
...Kumbe jini kisilani kaingia katika utamu wa penzi langu, alikuwa akiimba
...hapa alikuwa akimwaga mauno mbele ya mashabiki waliohudhuria.
Janeth Sostenes akifanya mahojiano na Godwin Gondwe.
...Aha! madansa wa Diamond wakiwajibika nae
Mashabiki wa kutosha wakifuatilia show.
...Diambond akiwajibika vilivyo
...Madansa wakiwajibika
...Safi sana
...Utata ulianzia hapa pale Dimond alishuka stejini na kwenda kwenye meza waliokuwa wamekaa akina Steve Nyerere na Mboni Masimba na ndipo alipopewa t-shirt ambayo kwa mujibu wa udadisi na uchunguzi wa kudadavua mambo uliofanywa na mtandao huu wa Kajuna Blog, ilisemekana kuwa t-shirt hiyo ilikuwa inapicha ya mwanadada ambaye alikuwa akitoa na Diamond kwa sasa. Na ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kumrusha roho Wema Sepetu.
...Mwanadada Mboni Masimba akimkabidhi Diamond t-shirt huku Steve Nyerere akimtunza, Diamond alikabidhiwa t-shirt ili aipeleke kwa mwanadada Jokate Mwegelo.
...Hapa akikabidhiwa t-shirt na kupewa maelekezo mahali pa kuipeleka.
...Baada ya hapo kumaliza lile 'movie' la kwanza aliendelea na kupita katika meza mbali mbali huku akiwasalimia wageni waalikwa.
...Akiimba na bendi ya Odama ambayo alimpa ushirikia mkubwa.
...Mauno yamekolea
...Akiendelea kutoa shukrani kwa wageni waliofika kumsapoti.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Q-chief akimpa sapoti mdogo wake Diamond
...Ehe! utata mkubwa ambao ulizuka ni hapa ambapo mwanadada huyu alianza kumtunza dola za Kimarekani, Diamond
...Diamond aliendelea kuimba wakati mwanadada huyo akimtunza kwa kutoa tabasamu na kicheko
Mwadada huyo hapa alikuwa amemaliza na kuondoka kwa mikogo...
Baada ya Diamond kurudi stejini ndipo mwanadada Wema Sepetu alienda kumtuza na pesa zake kukataliwa. Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10 japo zoezi lake halikufanikiwa.
...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza
...Bembeleza, bembeleza na wewe, ndiyo kwanza jamaa aliendelea kuwajibika
...alipoona amebembeleza bila mafanikio alichukua uamuzi wa kuzitupia pesa zile hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna
...Shamim Mwasha akilaumu kitendo alichokifanya Diamond cha kukataa hela alizoenda kutuzwa na Wema... Alisema, 'Haiwezekani hii ni aibu sana'
Pesa alizokataa kuzichukua Diamond zikiwa zimetupwa
...Hapa alipiga kitu cha 'Nimpende Nani'
...Jokate na marafiki zake wakishangilia
...Baada ya tukio hilo kutokea Mange Kimambi ambaye alikuwa ni mpambe wa Wema alimuita mshereheshaji wa tamasha hilo, Taji Liundi na kumuomba amuite Diamond ili aende kumuomba msamaha na ndipo Diamond akakataa.
...Diamond alishuka na kuelekea kwa mwanadada Jokate Mwegelo na kuanza kukata mauno.
...mwanadada Mboni Masimba akiwa amevaa t-shirt ambao zilileta utata.
...Aha! nimependeza sana
Taji Liundi akimbembeleza Diamond ili aende kwa Wema ndipo Diamond akakataa.
...Mwanadada Mariam (Miss Popular) akimfuta jasho Diamond wakati Taji Liundi akimbembeleza ili aende kwa Wema.
...Diamond akiserebuka na warembo
Marafiki wa Wema Sepetu wakijaribu kumbembeleza wakati akimwaga chozi... huku watu wengine wakishangilia na kuimba aibu yetu au aibu yao???
...hapa mwanadada akijaribu kubembeleza bila matumaini.
Msanii wa kizazi kipya, Ommy Dimpozzz akimpa sapoti Diamond...huku akitoa ushuhuda wa maisha yake na ya Diamond walipotoka.
...baada ya ujumbe wa Ommy Dimpozz, Diamond alimwaga chozi na hapa alikuwa akijifuta.
Amini nae hakuwa nyuma kumpa sapoti
...Barnaba, Amini na Diamond wakiwajibia
Baada ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda kumtuza na kutoa machungu yake. Kwa mujibu wa uchunguzi na maoni ya watu mbali mbali walikiona kitendo cha Wema Sepetu kwenda mbele kumtuza Diamond ni sawa na kujidhalilisha na kuhusishwa na mambo ya kishirikina.
Pia Justmine Loyce Bobbie alisema: Kwanini Wema anamfatafata mtoto wa watu kila kona? amuache na maisha yake jamani.. mbona Diamond hamfatilii lol, YATAMSHINDA
Upande wake; Veronica Stima alisema: Pale kilichokuwa kinatafutwa ni jinsi gani show ya Diamond 4ever iandikwe...hivyo akaona atafute 'lead' auze sura kwamba kamtunza Diamond kwa vile watu tunajua washapotezeana hivyo ni lazima story iiuzike na hakukubali kufunikwa na mdada alotoa dola kwa Diamond... mdada kafanikiwa though katika style ambayo hakuitegemea, usupastaa kazi make keshawapa watu cha kuongea... If I was here, ningechill tu hata mbele nisingesogea kwa vile what goes around, always come back around... ndiyo yanayotokea.. Big up kwa Diamond kwa vile kashow love mwanzo mwisho harafu hakujichetua mtoto wa kiume!!! Ili dunia izunguke watu kama kina Wema lazima wawepo so mwacheni aishi kadri impendezavyo nafsi yake.

RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA AfDB


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, akiomuonesha maendeleo ya ujenzi wa barabara nchini katika ramani ya Tanzania Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Mary Consolata Muduuli (wa pili kulia) Ikulu, Dar es Salaam, leo Machi 31, 2012. Bi. Muduuli ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Seychelles, Rwanda, Ethiopia na Eritrea, alifuatana na Mwakilishi wa Benki hiyo katika Tanzania. Bi. Tonia Kandiero ( wa pili kushoto) na mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, Bi. Salma M Salum. Picha na IKULU

DIAMONDS ARE FOREVER SHOW, MLIMANI CITY- DAR ES SALAAM


Dimond Are Forever show.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhyna Kusaga (kati) na mdogo wake.
Bendi ya Odama ikitumbuiza katika usiku wa Diamond Are Forever.
Wageni waalikwa.
...Mazungumzo ya hapa na pale yanaendelea.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhyna Kusaga (wa nne kulia) akiwa na marafiki zake na wageni waalikwa.
...Furanana vicheko vya hapa na pale.
...Marafiki wakipata picha
...raha, watu wakishow love

 

0 comments:

Post a Comment