Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Friday, March 2, 2012

UWOYA MIMBA NJE YA NDOA?Na Waandishi Wetu
GUMZO kubwa jijini Dar es Salaam kwa sasa ni madai kuwa Irene Pancras Uwoya ana mimba kwa mara nyingine huku mwanaye Krish akiwa na takribani miezi nane tu, Amani lina data kamili.
ISHU ILIANZA DESEMBA, MWAKA JANA
Madai ya Uwoya kuwa ‘ameshiba’ tena nje ya ndoa kabla hata Krish hajafikisha miezi nane, yalianza kuzagaa Desemba, mwaka jana, ‘kitumbo’ kikiwa na miezi takribani miwili.
ETI KITUMBO KINA ZAIDI YA MIEZI MINNE
“Tunapozungumza sasa hivi, ujauzito wa Uwoya umetimiza miezi minne, anaingia wa tano, kama mnataka ushahidi, mtafuteni mpate picha ya tumbo lake halafu mlinganishe na siku za nyuma baada ya kujifungua Krish,” alisema mmoja wa mashosti zake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina.

HAIONEKANI KAMA ILE YA KRISH
Ilidaiwa kuwa mwanzoni Uwoya hakugundua kama ilivyokuwa mimba ya Krish kwani hadi inatimiza miezi minne hakugundua chochote hadi alipokwenda kupima.

‘MMECHELEWA KUJUA’
Akizungumza na Amani kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, rafiki kipenzi wa Uwoya alionekana kushangazwa kwa kitendo cha gazeti hili kumhoji jambo ambalo limeshakuwa wimbo wa taifa.
“Ngoja niwachane laivu, kusema kweli mmechelewa kujua kwani wasanii wote wanajua ishu hiyo,” alisema rafiki huyo.

NI YA NJE YA NDOA?
Madai mengine ya kushtua ni kuwa mimba hiyo ni ya nje ya ndoa ambapo baada ya mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kuchezwa na machale, alilifikisha suala hilo kwa wazazi wa Uwoya ambapo familia ilikaa kikao.
“Janet (shosti wa Uwoya) alikuwepo kwenye kikao lakini alichomolewa kwa sababu fulani fulani, nasikia ni mmoja wa watu waliohusika kuvujisha ishu hiyo,” alisema mdaku wetu aliyenasa mkanda kamili.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa hadi kikao hicho cha saa kadhaa kinamalizika, hakikueleweka kufuatia Uwoya kutia ngumu kumtaja mhusika huku aking’ang’ania kuwa mwenye mali ni Ndiku.

ETI UWOYA ALISHAURIWA KUICHOROPOA, AKAGOMA
Kwa mujibu wa staa mkubwa wa kike wa filamu ambaye Uwoya anamheshimu (jina linahifadhiwa), mwanzoni mama Krish alishauriwa kufuata uzazi wa mpango kwa kuichoropoa mimba hiyo ili kuweka uwiano kati ya Krish na mtoto mwingine atakayezaliwa, lakini staa huyo aligoma.
“Uwoya anapenda sana watoto ‘so’ alikataa kuichoropoa na kama utakumbuka hivi karibuni aliliambia gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa atazaa mpaka basi kwa sababu anataka kuwa na kichanga kila mara.

UWOYA LAIVU
Baada ya ishu hiyo kuendelea kushika kasi mithili ya moto wa kifuu katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, Amani lilifanya mahojiano na Uwoya ambapo mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
Amani: Mambo vipi Uwoya?
Uwoya: Poa, najua kuna jambo ‘so’ ulizeni niwape ukweli wenu.


Amani: Kwanza hongera kwa ujauzito wa mdogo wake Krish.
Uwoya: Teh, teh, tehee! Nani kawaambia?
Amani: Habari zilizozagaa kila kona ya Jiji la Dar zinasema wewe ni mjamzito wa miezi minne unakwenda wa tano, je, ni kweli?


Uwoya: Mh! Yaani mtaani wanasema nina mimba? Naomba ieleweke kuwa sina ujauzito.
Uwoya aliyefunga ndoa na Ndiku mwaka 2009 na kujaliwa mtoto mmoja wa kiume mwaka jana, Krish, hakuwa tayari kufafanua juu ya ama mimba hiyo ni ya nje ya ndoa au la, zaidi ya kung’ang’ania kuwa hana kibendi.

0 comments:

Post a Comment