Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Monday, March 5, 2012

JANE MPONZI HATUNAE TENA

Marehemu Jane Mponzi
Nivigumu kuamini katika mazingira ya kawaida...lakini Ukweli ni kuwa Jane Mponzi (Mrs Herry Makange) hatunaye tena duniani.Hakika ni kifo na msiba wa kustua sana, Jane amefariki ghafla kama alivyofariki Mume wake Herry Makange miaka kadhaa iliyopita.Marehemu Jane amefariki leo Jumapili machi 4,2012 asubuhi kwa shinikizo la damu.Marehemu Jane Makange na Herry Makange enzi za uhai wao katika Send off ya Jane.Mengi yanaweza kusemwa lakini Ukweli utabaki pale pale kuwa Jane hatunae tena. Nimajonzi kwa kila amjuaye na anaemfahamu Jane. Binafsi ni juzi tu nilizungumza nae kwa kutaniana mimi na yeye kama kawaida yetu tunavyotaniana mtu na shemeji yake. kumbe ilikuwa ni simu yangu ya mwisho kumpigia na kuongea nae...Jane pumzika kwa amani na Mungu akupe faraja ya milele na Msalimie sana rafiki yangu Herry Makange naimani amekupokea kwa furaha sana.Blogu hii inatoa pole kwa Mtoto wako kipenzi, Familia ya Mzee Mponzi, Ndugu jamaa na marafiki zako wote na familia nzima ya Vodacom Tanzania.

Buruani Jane Mponzi.


0 comments:

Post a Comment