Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Saturday, January 7, 2012

ETI MTOTO WA IRENE SI WA NDIKUMANA BALI NI WA DUDE

Habari ya kuvunjika kwa ndoa ya Irene Pancras Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’, inazidi kuibua mapya kila kukicha ambapo inadaiwa kuwa, eti mtoto wao siyo zao la mwanasoka huyo wa Kimataifa wa Rwanda.
MADAI YALIANZA KITAMBO
Tangu mtoto huyo alipoanza kuonekana kwenye vyombo vya habari, siku chache baada ya kuona jua Mei, 2011, kumekuwa na maneno ya tuhuma nzito kuwa siyo kopi ya jamaa huyo.
YUPO KIGOGO SERIKALINI
Tuhuma hizo sasa zinachukua kasi mithili ya moto wa kifuu huku wakitajwa mastaa kama akina Kulwa Kikumba ‘Dude’ na kigogo mmoja serikalini ambaye pia ni mdau mkubwa wa burudani Bongo (jina tunalo, tutamtaja baadaye).
RISASI JUMAMOSI MZIGONI
Baada ya madai hayo kukolea, mwezi Novemba, mwaka jana ndoa hiyo ilipopigwa kimbunga mara ya kwanza, Risasi Jumamosi liliwatafuta wahusika wote kwa nyakati tofauti ili kupata mzani wa madai hayo.
ALICHOKISEMA DUDE
“Irene (Uwoya) ni mwigizaji mwenzangu, kama chanzo cha madai hayo ni kuonekana na mrembo huyo, ieleweke kwamba tulikuwa tunafanya filamu pamoja.
“Baada ya kumaliza kazi kila mtu alichukua hamsini zake. Hakuna kitu kama hicho, jumba bovu lisiniangukie mimi.
“Lakini mtoto si yupo? Ampeleke hospitali akapime DNA (vinasaba) ataamini maneno yangu, yanini kuandikia mate?”


HEBU MSIKIE KIGOGO SERIKALINI
“Ni kweli nafahamiana na Irene (Uwoya), lakini hilo mnaloniuliza mnalenga kunidhalilisha. Si kweli hata kidogo.”


UWOYA LAIVU
“Ni kweli anayejua baba wa mtoto ni mama. Ninachokijua mimi mtoto ni wa Hamad (Ndikumana).
“Hao wanaotajwa nafahamiana nao kama waigizaji wenzangu na marafiki tu, hakuna kitu ka’ hicho.
“Duh! Ama kweli watu wana maneno, hivi huwa wanayatoa wapi?

0 comments:

Post a Comment