Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Thursday, December 29, 2011

hekaheka za sikukuu

 
Katika msimu huu wa kusherehekea sikukuu ya Noel (Christmass), baadhi ya mastaa wa Kibongo wamekumbwa na kizaazaa na kutiwa mbaroni.
Hao si wengine bali ni Wema Isaac Sepetu ‘Mama Diamond’, Kajala Masanja na Mtangazaji wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida wa G’.
NYUMA YA NONDO OYSTERBAY
Mastaa hao walikaa polisi nyuma ya nondo kwenye Kituo cha Osterbay, Dar es Salaam Ijumaa wiki iliyopita, chanzo ni kumshambulia Christina John Manongi ‘Sintah’ usiku wa Alhamisi iliyopita.

WAZUA TIMBWILI
Habari zilizotua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda zilidai kuwa, mastaa hao, wakiwa na mwanamke mmoja wa mjini aliyetajwa kwa jina moja la Jennifer, walidaiwa kuzua timbwili la maana kwa kumfanyia fujo Sintah nje ya Ukumbi wa Polisi Officers Mess Masaki, Dar alipohudhuria kitchen party ya Mtangazaji wa Star TV, Sauda Said Mwilima.

JOKATE TENA
Ilisemekana sosi ya kumkosakosa Sintah huku akiambulia ‘masingi’ ya kutosha ni madai kuwa muigizaji huyo wa kitambo alichafua hali ya hewa baada ya kutangaza kutoa zawadi kwa Mwilima kwa niaba ya Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo ambaye kwa sasa ni hasimu wa Wema kisa penzi la Naseeb Abdul ‘Diamond’.

SINTAH AKOSWAKOSWA
Habari zilizidi kusambaa kama moto wa kifuu kuwa baada ya Sintah kutoa kauli hiyo, ndipo Wema na wenzake walipomvizia nje na kutaka kumkong’ori na kutishia kuvunja vioo vya gari lake.
Baada ya kunusurika kufanyiwa ‘ugadafi’ huo, Sintah aliamua kukimbilia kwa vijana wa Kova ambapo alifungua jalada la kesi namba OB/RB/22598/11-SHAMBULIO.

MIKONONI MWA POLISI
Bila kupoteza muda, polisi walifanya kazi yao na kuwatia mikononi wahusika wote.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
‘Kipande’ cha gazeti hili kilijipeperusha hadi kituoni hapo na kuwashuhudia mastaa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali.

NUSURA WALE SIKUKUU KOROKORONI
Kwa kuwa walifikishwa kituoni hapo siku ya Ijumaa, ilibidi kufanya kazi ya ziada ili kufanikisha dhamana kwani wangekula Krismasi mahabusu hadi Jumanne (kesho).

DHAMANA
Hata hivyo, Mungu si Athumani kwani walifanikiwa kuwekewa dhamana ambapo upelelezi unaendelea.

WATAFUTA NAMNA YA KUJINASUA
Habari za kipekepeke zilidai kuwa

0 comments:

Post a Comment