Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Friday, December 2, 2011

BREAKING NEWS: Mr Ebo Afariki Dunia!

Aliyekuwa mwanamuziki, producer na mmiliki wa studio za Motika records za jijni Tanga, Abel Motika a.k.a Mr. Ebbo, amefariki dunia jana mida ya saa 3 usiku akiwa hospitali ambapo inaelezwa alikuwa akiumwa.
Ebbo atakumbukwa enzi hizo alipotamba ile mbaya na wimbo wake 'Mi Mmsai' , uliotokea kupendwa na mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva ukanda huu afrika mashariki.
Habari zinaeleza kwamba Mr. Ebbo alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na amefarikii akiwa nyumbani kwake Mkoani Tanga.
Mipango ya kuusafirishwa mwili wa Marehemu kuelekea Jijini Arusha kwa mazishi inafanyika kwani anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu nyumbani kwa baba yake Boma karibu na Masai Kempu.
Hakika katangulia nasi twafwata nyuma , Bwana alitoa na Bwana ametwaa.

0 comments:

Post a Comment