Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Loading...

Friday, November 18, 2011

mimba ya lady jay dee


 TANGU alipolazwa hivi karibuni hospitalini nchini Ufaransa akisumbuliwa na ugonjwa aliodai ni wa ‘heri’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, amekuwa gumzo mitandaoni na neno pekee linalotajwa ni mimba!... mimba!

The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda limekuwa likifuatilia kwa ukaribu habari hizo huku staa huyo mkubwa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo akiombwa chondechonde kueleza ukweli.

APANGUA MAONI YA MASHABIKI WAKE
Kupitia mtandao wake, Lady Jaydee a.k.a Jide amekuwa akipangua maoni yanayotolewa na mashabiki wake kupitia mtandao huo huku baadhi wakimpongeza kwa kuwa mjamzito.

“Kila comment ninayofungua, mimba…mimba…hata kama mada haihusiani,” alijibu Jide akipangua maoni hayo na kuongeza:
“Sasa naanza kuzoea wimbo huu wa mimba…mimba...”

Ijumaa Wikienda linashikilia maoni zaidi ya 1,000 ya mashabiki wake waliokuwa wakimhoji juu ya kuwa mjamzito hasa baada ya kulazwa na kusema kuwa ni ugonjwa wa heri.
Mfano wa maoni hayo ni: “Hongera Binti Machozi (Lady Jaydee), ni kweli una mimba?”

APOKEA PONGEZI
Pamoja na kupokea pongezi bila kusema kama kweli ni mjamzito au la, Jide aliwataka mashabiki wake kusubiri hadi hapo watakaposikia kutoka kwake.
“Naomba msubiri kusikia kutoka kwangu…” ilisomeka sehemu ya majibu ya Jide.

MJAMZITO?
Mwezi Septemba, mwaka huu Jide alitangaza kuwa kwenye ‘dayati’ kwa ajili ya kuweka umbile lake bomba ikiwa ni pamoja na kuondoa tumbo.


Zoezi hilo lilifanikiwa kwa asilimia nyingi, lakini ghafla staa huyo anayemiliki Machozi Band alianza kutokwa na kitumbo kiaina, jambo lililozidisha furaha kwa mashabiki wake.
“Judy (Jide), mbona kitumbo kinakua kila kukicha? Umeacha dayati?” Yalisomeka maoni ya shabiki wake mtandaoni.

AMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO
Hivi sasa kwenye mtandao wa staa huyo hakukauki neno la Mungu na mada za ujauzito.
“Mungu ni mkuu, amenitendea makubwa,” alisema Jide anayevaa mavazi meupe kwa mwezi huu wa Novemba wote na kuongeza:
“Sikukata tama kama wengine...”

MADA ZA UJAUZITO
Kilichochochea mjadala zaidi ni mada anazozitoa Jide ambaye ni mke wa ndoa wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds, Gardner G. Habbash kupitia mtandao wake.
Aliandika: “Kumpiga mwanao akiwa tumboni ni sawa na kunywa pombe wakati wa ujauzito.”

GARDNER VIPI?
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumdodosa Gardner ambaye hivi karibuni alisafiri na kwenda kuungana na mkewe nchini Ufaransa kuhusiana na ishu hiyo, lakini ilishindikana.

Wiki mbili zilizopita, Jide anayemiliki Mgahawa wa Nyumbani Lounge, Dar es Salaam aliripotiwa kulazwa kwa ugonjwa usiojulikana
.

0 comments:

Post a Comment