Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Saturday, October 8, 2011

Sukari kutoka nje kuanza kumiminika nchini karibuni

Mchakato wa kuyapata makampuni yenye uwezo wa kuagiza sukari nje ya nchi umekamilika na sasa muda wowote yataanza kufanya kazi hiyo ili kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini. Hata hivyo, kumekuwa na usiri mkubwa kutoka Bodi ya Sukari Tanzania ambayo inasimamia mchakato huo ambapo imegoma kuweka wazi idadi ya makampuni yaliyopitishwa juzi katika kikao maalumu kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya bodi hiyo, tayari makampuni hayo yameishapitishwa kwa kuangalia vigezo mbalimbali na muda wowote yatapewa leseni ili yaanze kuagiza sukari bila ya kulipia ushuru. Wakati serikali ikitangaza kuyapa makampuni binafsi kazi ya kuagiza sukari nje ya nchi iliahidi kuwepo uwazi katika mchakato huo ili kila mwananchi ajue kinachoendelea. Hata hivyo, ghafla hali hiyo imebadilika na kuonekana kuwa zoezi hilo ni la siri kubwa. Kikao cha kamati iliyopitisha majina hayo kilijumuisha wajumbe kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Bodi ya Sukari, Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wazalishaji wa Sukari na TCCIA. Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Mathew Kombe, jana kutwa nzima hakupatikana ofisini kwake ili kutoa orodha ya majina hayo na kuelezea mipango mingine baada ya zoezi hilo kukamilika. Makampuni 40 yaliwasilisha maombi serikalini kutaka yapewe kazi ya kuagiza sukari ambapo Septemba 30, mwaka huu, ilikuwa siku ya mwisho ya kuyapokea. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema mwezi uliopita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mohamed Muya. alisema serikali itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi ambapo haitalipiwa kodi. Alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao kilichoshirikisha Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara wa Viwanda, Biashara na Masoko, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Fedha na Uchumi. Muya alisema kampuni hizo pia zitaruhusiwa kuagiza sukari kutoka katika nchi yoyote ambayo zitaona ni rahisi kupata bidhaa hiyo ili mradi iwe rahisi kuifikisha hapa nchini na kuwafikia watumiaji

0 comments:

Post a Comment