Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Tuesday, September 20, 2011

Mume aua mke naye ajiua kwa wivu

MUME anadaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi kifuani kisha na yeye kujipiga risasi mdomoni na kufia hospitalini kutokana na ugomvi unaodaiwa kusababishwa na wivu wa mapenzi.

Wanandoa hao, Boniface Anthony mwenye umri wa kati ya miaka 55 na 60 na mkewe, Sauda Omari (35) ambao ni wakazi wa Kijiji cha Kwabada wilayani Muheza, katika Mkoa wa Tanga, walifariki dunia juzi saa 4 usiku.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanandoa hao ambao ni wakulima wa kijiji hicho, walikuwa na ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi.

Hata hivyo haikufafanuliwa chanzo halisi. “Tumefahamishwa kwamba siku hiyo ya tukio Anthony alimpiga mkewe Sauda risasi za kifuani na kumsababishia kifo papo hapo na mara baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi za mdomoni ambazo zilimfumua taya na kichwa ila
alipata msaada wa kufikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu”, alisema.

Kamanda alisema pamoja na jitihada hizo, Anthony alifariki kwenye Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza wakati akiendelea na matibabu.

Miili iko kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini ikisubiri ndugu kufanya taratibu za maziko. Kwa mujibu wa Kamanda, mauaji hayo yalifanyika kwa kutumia bunduki aina ya Shot gun yenye namba za usajili G 71289 ambayo Anthony alikuwa akiimiliki kisheria.

0 comments:

Post a Comment