Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Monday, September 19, 2011

Mashambulio mapya yaanza Libya

Mashambulio mapya yaanza Libya

Majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya aliyeondolewa Kanali Muammar Gaddafi yameanza mashambulio mapya kwenye mji wa Bani Walid.
Wanaomtii wamekuwa wakirusha makombora na kutumia wadunguaji kuyalenga majeshi yanayompinga Gaddafi kwenye lango la kaskazini la mji huo.
Libya
Majeshi yanayompinga Gaddafi yanasonga taratibu katika ngome nyingine ya wanomtii - mji wa pwani wa Sirte.
Wakati huo huo, baraza la mpito la taifa, uongozi wa mpito wa Libya, unajadili kuhusu baraza jipya la mawaziri.
Taarifa kutoka Bani Walid zinasema milipuko na milio ya risasi yamekuwa yakisiskika nyakati za asubuhi baada ya majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi kurusha makombora.

0 comments:

Post a Comment