Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Monday, September 19, 2011

Fumanizi-ingawa wakana


Fumanizi Lipi? -Aunt Ezekiel Mastaa wa muvi za Bongo, Aunt Ezekiel na Steven Kanumba wametegua utata wa fumanizi lililodaiwa kuwatokea Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Wawili hao waliamua kufungukia uvumi huo walipoongea na mwandishi wetu hivi karibuni huku ishu ikidaiwa kutokea wiki mbili zilizopita.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunt alisema kuwa siku hiyo hakukuwa na aina yoyote ya fumanizi ingawa alikiri yeye, Kanumba na wasanii wengine, akiwemo Ray kuwepo kwenye Viwanja vya Leaders.

Alisema kuwa, siku hiyo alikwenda kwenye viwanja hivyo kujumuika na mastaa wenzake hao huku wakipata vinywaji mbalimbali kama vile pombe.

Aunt aliendelea kuanika kwamba, wakiwa katikati ya starehe yao, palitokea kutoelewana kati yake na Kanumba na kusababisha tafrani ambayo haikuwa kubwa kwa vile baadhi ya watu waokuwepo walisuluhisha.
Akasema kuwa, baada ya siku hiyo akashangaa kusikia maneno mitaani kwamba, boifrendi wake alimfumania akiwa chobingo na Kanumba.

“Mimi hilo sula la fumanizi sijui lilikotokea kwa sababu mimi na huyo mtu (Kanumba) ni mtu ambaye tumezoeana sana, si rahisi kufanya kitu kama hicho,” alisema Aunt.
Msanii huyo aliongeza kuwa si mara ya kwanza yeye kuandamwa na kashfa ya mapenzi na Kanumba na kwamba anajua yote inatokana na kuzoeana kupita kiasi kwa sababu ukaribu wao unatokana na kucheza  filamu.

“Ni kazi zetu ndiyo zinatufanya tusogezane karibu  mpaka watu kuanza kusema vitu ambavyo havina manufaa wala uhakika,” alisema Aunt.

Kwa upande wake, Kanumba alipopatikana kwa njia ya siku ya kiganjani naye alikana kufumaniwa na Aunt lakini alikiri siku inayotajwa kwamba tukio lilitokea, alikuwepo Leaders na washkaji zake na si kwa ahadi na Aunt.

“Hakuna kitu kama hicho, sijafumaniwa na Aunt, hiyo siku nilikuwa Leaders kweli, lakini si kwa sababu ya huyo demu (Aunt), watu ni wazushi tu,” alisema Kanumba.
Tetesi za wawili hao kufumaniwa zilizagaa jijini Dar siku moja baada ya siku  wanayokiri kuwepo Leaders.

Baadhi ya watu wa karibu na mastaa hao wamekuwa wakizungumza maoni tofauti kuhusu madai hayo ambapo wapo waliodai na wao wamesikia hivyo, wengine wakikataa.

0 comments:

Post a Comment