Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Monday, September 19, 2011

ANAYETUMIA JINA LA LULU FACEBOOK,AMDHALILISHA IRENE UWOYA KUPIGA PICHA ZA X.!M


MTU anayetumia jina la Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) katika mtandao wa kijamii wa Facebook, amesababisha kisanga kati ya muigizaji mwenye jina hilo na mwenzake, Irene Pancras Uwoya, Ijumaa linafunguka.

Mtu huyo anashutumiwa kumchafua na kumdhalilisha vibaya Uwoya huku akitamba kwamba yuko tayari kutumia maumbile ya mwili wake wote kucheza muvi chafu ya ‘X’.AMDHALILISHA UWOYA, MUMEWE NA MWANAYE

Katika ukurasa wake, Lulu huyo aliandika maneno makali yasiyochoreka gazeti yakimkashifu Uwoya na familia yake.

Katika maelezo yake, mtu huyo alijisifu kuwa ana maumbile ‘seksi’ hivyo muda si mrefu atasukuma sokoni filamu yake chafu ya ngono na kuwataka watu wakae mkao wa kula.

MSHANGAO MKUBWA
Matusi na tambo za Lulu huyo ziliibua mshangao mkubwa kwa mashabiki wengi wa wasanii hao wanaotikisa katika anga la filamu za Kibongo huku baadhi wakidai kuwa inawezekana ndiyo tabia zao.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, The Udaku Master, Ijumaa lilimwinulia mkonga wa simu Lulu ‘orijino’ na kumbana juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: “Ukweli ni kwamba huyo mtu nimemchoka kabisa, aliwahi kunigombanisha na Zamaradi (Mketema).

“Sijawahi kumkosea heshima Uwoya, namuomba awe mvumilivu, ampuuzie huyo mtu kwani hata tukisema tumsake ni vigumu kumpata. Kwanza nasikia ni mwanaume.”

UWOYA ANASEMAJE?
Kwa upande wake, Uwoya ‘Oprah’ ambaye yuko nchini Burundi kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza alikuwa na haya ya kusema juu ya kisanga hicho:
“Ukweli ni kwamba hata hiyo Facebook yenyewe sijaingia ‘so’ ngoja niingie mara moja.”
Baada ya muda, Uwoya aliendelea kufunguka:

“Nitajaribu kumtafuta Lulu kwenye simu nisipompata nikirudi Tanzania nitakutana naye nijue ni yeye aliyeandika au mtu tu anatumia jina lake. Nadhani tutaweka mambo sawa.”
Facebook imeendelea kuwa chanzo cha watu mashuhuri kuchafuliwa majina hivyo watumiaji wake wanapaswa kuwa na roho ya utu kwa wale wanaowachafua.

0 comments:

Post a Comment