Subscribe:

Ads 468x60px

.

Tafuta Kila kitu Hapa

Friday, September 16, 2011

ajali ya ndege angola

Ajali ya ndege Angola yaua majenerali

Ajali ya ndege nchini Angola imesababisha vifo vya watu 26, wakiwemo majenerali wa kijeshi watatu, afisa wa serikali ameiambia BBC.
Luis Caetano, msemaji wa mamlaka ya jimbo la Huambo, alisema ndege hiyo ya kijeshi ilianguka baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Huambo.
Alisema watu sita waliokoka kwenye ajali hiyo, akiwemo rubani na msaidizi wake.
Waandishi wa habari wamesema ni ndege mpya ya muundo wa Embraer iliyonunuliwa na jeshi kusafirisha maafisa waandamizi.
Taarifa za awali zilisema kulikuwa na abiria 36, lakini Bw Caetano ameiambia BBC walikuwepo 32.
Alisema ndege hiyo ilipasuka ilipopata ajali hiyo na miili ya watu 26- 20 ya wanaume na sita ya wanawake iliopolewa.
Watu waliokuwa wamekaa sehemu ya mbele ya ndege hiyo walinusurika, lakini waliokaa nyuma walifariki dunia kutokana na upande huo kushika moto.
Bw Caetano alisema, mmoja wa walionusurika aliungua sana na alikuwa akipata matibabu hospitalini.
Alisema, rubani aliyezungumza na televisheni ya Angola, alionekana kuchanganyikiwa lakini alisistiza kuwa alifuata masharti yote aliyopewa.
Mmoja wa walionusurika alinukuliwa na gazeti la Sol akiwa hospitali akisema ajali hiyo ilitokea haraka kiasi cha kushindwa kujua tatizo ilikuwa ni nini, lakini rubani alionekana kufahamu kwamba kulikuwa na tatizo la kiufundi.

0 comments:

Post a Comment